Skip to main content

UMUHIMU WA KARAFUU

UMUHIMU WA KARAFUU KATIKA AFYA YAKO.

Karafuu ni kiungo na dawa muhimu sana na yenye thamani kubwa amabacho kimetumika kwa karne nyingi kutibu matatizo ya kumeng'enya chakula na mfumo wa kupumua kwa binadamu. Ina wingi wa vitamini A,C,K na B-complex' na madini muhimu kama 'manganese', 'selenium, 'iron', 'potassium' na 'magnesium'. Ina nguvu nyingi katika kupambana na maambukizo vya virusi, fungasi na bacteria ambazo huzuia jeraha mbichi kuvimba na pia kupoza maumivu wakati unapata jeraha. Sifa hii hufanya karafuu kuwa muhimu katika tiba ya maradhi mengi.
Karafuu husaidia mfumo wa kumeng'enya chakula, gesi sugu, kukosa choo, kuvimba tumbo, kichefuchefu na matatizo yanayoletwa na vyakula vyenye viungo vingi ili vyakula vile visidhuru mwili. Huondoa maumivu ya misuli,kuumwa na kichwa na maumivu ya neva. Pia hutumika kuua vidudu katika fizi, meno, ini, pafu, ngozi na mishipa ya kupumulia.Mafuta ya karafuu yana kichocheo cha 'eugenol' ambacho kina nguvu ya kupooza na kuondoa maumivu na harufu mbaya mdomoni.Hivi huifanya kutumika kupoza maumivu na kuondoa maumivu hasa ya meno na fizi. Mafuta ya karafuu pia ni muhimu katika mfumo wa mzunguko wa damu na kuzuia damu kuganda. Pia hutumika kutibu miguu kuvimba, kutibu vidonda, vipele, mikwaruzo na kuchomeka.
Ukifukiza mafuta ya karafuu kama unavyofukiza udi na uyanuse yale moshi inapunguza makali ya matatizo ya kupumua kama 'sinusitis', 'TB', 'bronchitis', 'asthma', mafua makuu na kukohoa,
Karafuu huchanganywa na viungo vyengine kutengeneza mchanganyiko ambao hutumika kupikia chakula kama 'Curry Powder na Garam Masala barani India na hata huku Afrika mashariki. Chai ya karafuu inasaidia kuupa nguvu mfumo wa kinga na kuondoa sumu mwilini. Weka vijiko viwili vya karafuu ndani ya vikombe viwili vya maji chemsha kwa dakika 10 funika, wacha itulie kama dakika 8, tia na kijiko cha asali ili upate faida zaidi.
Karafuu hupatikana masokoni au katika maduka ya viungo. Pia ipo katika mfumo wa vidonge, mafuta, chai yake na cream ambazo unaweza agiza kwenye mtandao au maduka ya dawa.

Comments

Popular posts from this blog

MAUMIVU YA WAKATI WA HEDHI

MAUMIVU WAKATI WA HEDHII Wapo baadhi ya akina mama wao hupatwa na maumivu makali mno,wanapokuwa katika ada zao za kutokwa na damu ya hedhi kama na wewe ni mmojawapo nakushauri tumia dawa hii kisha ulete maendeleo yako .............................................. Chukua NANAA kiasi cha robo kg ichemshe kwa maji lita2 na nusu hakikisha inachemka hadi maji hayo yabaki lita2 tuu Anywe mdada huyu anayepatwa na maumivu ya hedhi kikombe kimoja cha chai kutwa mara 2 ni vizuri zaidi akitumia kipndi ambacho anaona dalili ya kuingia hedhini MAUMIVU YATAKUACHA. ☎️ Kwa mawasiliano zaidi na maelekezo zaidi tupigie SULLE NATURAL MEDICINE CLINIC 0655589502, 0715589502, 0754589500 WHATSAPP 0714567151 Nyote mnakaribishwa.

MAUMIVU YA KICHWA

MAUMIVU YA KICHWA Maumivu ya kichwa hutokea watu wengi sana wa umri wote. Ni dalili inayopelekea watu wengi kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu. Kuna sababu nyingi zinazosababisha maumivu ya kichwa. Nyingi zikiwa zisizohatarisha maisha ya mtu, na baadhi zikiwa hatari kwa uhai wa mtu. Maumivu ya kichwa yanaweza kuwa ya kuanza mara moja ghafla (acute headache) au maumivu ya muda mrefu yanayokuja na kuacha (chronic headache). Dalili ambazo zinaweza kuambatana na maumivu ya kichwa ni homa, kutapika, kizunguzungu, moyo kwenda mbio, kupoteza fahamu, kutoona vizuri, kupata degedege na nyingine. Kwa kawaida unapopata maumivu ya kichwa onana na daktari wako kwa matibabu. Ikiwa maumivu ya kichwa yanaambatana na dalili zifuatazo basi wahi haraka sana hospitali iliyo karibu na wewe. Kuona vitu viwili viwili au giza, kupata degedege (convulsions), kupoteza fahamu, kutapika sana na moyo kwenda mbio. SABABU ZA MAUMIVU YA KICHWA • Malaria • Ajali ya kichwa • Matatizo ya macho • Damu kuvuja kwenye u...