Skip to main content

MAUMIVU YA KICHWA

MAUMIVU YA KICHWA

Maumivu ya kichwa hutokea watu wengi sana wa umri wote. Ni dalili inayopelekea watu wengi kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu. Kuna sababu nyingi zinazosababisha maumivu ya kichwa. Nyingi zikiwa zisizohatarisha maisha ya mtu, na baadhi zikiwa hatari kwa uhai wa mtu. Maumivu ya kichwa yanaweza kuwa ya kuanza mara moja ghafla (acute headache) au maumivu ya muda mrefu yanayokuja na kuacha (chronic headache).

Dalili ambazo zinaweza kuambatana na maumivu ya kichwa ni homa, kutapika, kizunguzungu, moyo kwenda mbio, kupoteza fahamu, kutoona vizuri, kupata degedege na nyingine.

Kwa kawaida unapopata maumivu ya kichwa onana na daktari wako kwa matibabu. Ikiwa maumivu ya kichwa yanaambatana na dalili zifuatazo basi wahi haraka sana hospitali iliyo karibu na wewe. Kuona vitu viwili viwili au giza, kupata degedege (convulsions), kupoteza fahamu, kutapika sana na moyo kwenda mbio.

SABABU ZA MAUMIVU YA KICHWA

• Malaria
• Ajali ya kichwa
• Matatizo ya macho
• Damu kuvuja kwenye ubongo
• Shinikizo la damu la kupanda
• Uvimbe kwenye ubongo
• Upungufu wa damu
• Upungufu wa maji mwilini
• Kifafa
• Gesi kujaa tumboni
• Kukosa usingizi
• Msongamano wa mawazo (depression au stress)
• Nguvu za giza (Uvamizi wa Jini)

MAGONJWA YA KUAMBUKIZA KAMA;
• Malaria
• Homa ya UTI wa mgongo
• Homa ya tumbo
• Ugonjwa wa toxoplasmosis

VIPIMO

Vipimo vinavyofanyika kutokana na maumivu ya kichwa hutegemea na chanzo chake. Vipimo hivi husaidia kugundua chanzo cha maumivu ya kichwa ili yatibiwe. Baadhi ya vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika.

1-- Kipimo cha damu cha malaria au homa ya tumbo (typhoid)
2-- Wingi wa damu (haemoglobin concentration)
3-- Kipimo cha maji ya mgongo (Lumbar puncture)
4-- X-ray ya kichwa
5-- CT Scan ya kichwa
6-- MRI ya kichwa

MATIBABU KUPITIA NJIA ZA HOSPITALI

Maumivu ya kichwa hutibiwa na kuisha pale ambapo chanzo chake kimejulikana na kudhibitiwa. Pale ambapo chanzo hakijajulikana, dawa za kutuliza maumivu hupunguza ukali lakini baadae yanaweza kujiridua tena. Dawa za NSAID kama 'Diclofenac' na 'paracetamol' hutumika kutuliza maumivu huku matibabu mengine yakiendelea. Kwa baadhi ya hali zinazosababisha maumivu ya kichwa huitaji matibabu yanayoweza kuhusisha upasuaji.

Wakati mwingine maumivu ya kichwa yanaweza kutokana na msongo wa mawazo, uchovu wa mwili na mambo mengi ya maisha. kwa kuzingatia yafuatayo:

-🌻 Kunywa maji mengi kila siku, zisipungue lita 2.5 au glasi 10 kwa siku moja. Itakusaidia kupunguza uchafu mwilini na ubongo upate damu ya kutosha.
-🌻 Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa nusu saa. Huimarisha kinga ya mwili wako, mzunguko wa damu na ukakamavu.
- 🌻Kupata mlo wenye virutubisho vya kutosha.
-🌻 Pata muda wa kupumzika wa kutosha, angalau masaa 8 ya kulala wakati wa usiku.
- 🌻Pata muda wa kutulia na kutafakari kuhusu maisha yako, kupanga mipango yako na kutuliza nafsi yako.
-🌻 Pata muda wa kuwa na rafiki zako, ndugu na jamaa unaowapenda.
-🌻 Ikiwa sababu ya kuumwa kichwa ni kutokamana na nguvu za giza (jini) tafta mwalimu akusomee ruqya (exorcism) ya halali bila kufanya ushirikina.

JE! UMEKUWA UKIUMWA NA KICHWA KWA MDA MREFU NA UMEFANYA VIPIMO HUSIKA BILA MAFANIKIO? 

👉BASI WASILIANA NASI ILI KUPATA TIBA MBADALA ZA ASILI KATIKA HOSPITALI YETU ILIYOPO DAR, SULLE NATURAL MEDICINE CLINIC

Tunapatikana kwa namba 0655589502, 0715589502, 0754589502 whatsapp 0714567151

Comments

Popular posts from this blog

UMUHIMU WA KARAFUU

UMUHIMU WA KARAFUU KATIKA AFYA YAKO. Karafuu ni kiungo na dawa muhimu sana na yenye thamani kubwa amabacho kimetumika kwa karne nyingi kutibu matatizo ya kumeng'enya chakula na mfumo wa kupumua kwa binadamu. Ina wingi wa vitamini A,C,K na B-complex' na madini muhimu kama 'manganese', 'selenium, 'iron', 'potassium' na 'magnesium'. Ina nguvu nyingi katika kupambana na maambukizo vya virusi, fungasi na bacteria ambazo huzuia jeraha mbichi kuvimba na pia kupoza maumivu wakati unapata jeraha. Sifa hii hufanya karafuu kuwa muhimu katika tiba ya maradhi mengi. Karafuu husaidia mfumo wa kumeng'enya chakula, gesi sugu, kukosa choo, kuvimba tumbo, kichefuchefu na matatizo yanayoletwa na vyakula vyenye viungo vingi ili vyakula vile visidhuru mwili. Huondoa maumivu ya misuli,kuumwa na kichwa na maumivu ya neva. Pia hutumika kuua vidudu katika fizi, meno, ini, pafu, ngozi na mishipa ya kupumulia.Mafuta ya karafuu yana kichocheo cha 'eugenol' a...

MAUMIVU YA WAKATI WA HEDHI

MAUMIVU WAKATI WA HEDHII Wapo baadhi ya akina mama wao hupatwa na maumivu makali mno,wanapokuwa katika ada zao za kutokwa na damu ya hedhi kama na wewe ni mmojawapo nakushauri tumia dawa hii kisha ulete maendeleo yako .............................................. Chukua NANAA kiasi cha robo kg ichemshe kwa maji lita2 na nusu hakikisha inachemka hadi maji hayo yabaki lita2 tuu Anywe mdada huyu anayepatwa na maumivu ya hedhi kikombe kimoja cha chai kutwa mara 2 ni vizuri zaidi akitumia kipndi ambacho anaona dalili ya kuingia hedhini MAUMIVU YATAKUACHA. ☎️ Kwa mawasiliano zaidi na maelekezo zaidi tupigie SULLE NATURAL MEDICINE CLINIC 0655589502, 0715589502, 0754589500 WHATSAPP 0714567151 Nyote mnakaribishwa.